TANGAZO LA AJIRA

Chuo cha Madini Shinyanga (ESIS), kinawatangazia wananchi wote wenye sifa nafasi ya ajira ya Mkufunzi wa Sayansi Asilia 01 (Natural Sciences-Tutor). Hivyo wahitimu wote kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 11 Disemba, 2023 hadi 29 Disemba 2023. Nafasi iliyopo ni kwa wahitimu kuanzia elimu ya shahada ya kwanza na kuendelea.

1.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI

1.1 Nafasi ya Mkufunzi wa Sayansi Asili 01 (Natural Sciences-Tutor).
i. Awe na Elimu kuanzia ngazi ya shahada, katika fani ya elimu masomo ya fizikia, kemia na hesabu au taaluma nyingne zihusianazo na sayansi asilia.
ii. Awe na vyeti kamili kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali katika mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha kidato cha nne, sita pamoja na cheti cha Taaluma ya fani aliyosoma).
iii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine;
iv. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kupatikana na hatia ya kosa la jinai;
v. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa raia wa Tanzania; na
vi. Aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

2.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi zingine watakazopangiwa;
ii. Waombaji wote wahakikishe wanatuma fomu za maombi na kuambatanisha nyaraka zote muhimu;
iii. Maombi ya ajira ni bure.

Kwa maelezo Zaidi kuhusu chuo tembelea tovuti ya chuo www.esis.ac.tz
Maombi yatumwe kwa njia ya barua pepe [email protected] mwisho wakupokea maombi ni tarehe 29 Disemba, 2023 saa 05:59 usiku.tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo: www.esis.ac.tz

Limetolewa na: Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Madini Shinyanga (ESIS),
S.L.P 1016,
SHINYANGA.


Pin It on Pinterest