Chuo cha Madini Shinyanga (ESIS), kinawatangazia wananchi wote wenye sifa nafasi ya ajira ya Msimamizi wa Wanafunzi (Warden). Hivyo wahitimu wote kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 10-20 septemba, 2023. Nafasi
iliyopo ni kwa wahitimu kuanzia elimu ya shahada na kuendelea.

1.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI

1.1 Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:

i.  Awe raia ya Tanzania;
ii. Awe na umri usiopungua miaka 25;
iii. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha kidato cha nne, sita
pamoja na cheti cha Taaluma ya fani aliyosoma.
iv. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine;
v. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kupatikana na hatia ya kosa la jinai;
vi. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
vii. Aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

2.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi zingine watakazopangiwa;
ii. Waombaji wote wahakikishe wanatuma fomu za maombi na kuambatanisha nyaraka zote
muhimu;
iii. Maombi ya ajira ni bure.
Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa mombi,
wasiliana nasi kupitia namba za simu +255 765 434 604 au +255 687 434 617.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Barua pepe [email protected] au [email protected]
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20 septemba, 2023 saa 05:59 usiku. Tangazo hili
linapatikana katika tovuti ifuatayo: www.esis.ac.tz.

Pin It on Pinterest