Jinsi ya kupata mkopo wa Elimu ya Chuo Tanzania
Mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Stashahada Tanzania
- Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo
wa mwaka wa masomo 2023/2024; - Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne
atakayoitumia mwombaji iwe sawa na aliyoombea udahili
wa chuo; - Kuhakikisha kuwa fomu ya maombi ya mkopo na mkataba
zimesainiwa na viongozi wa serikali ya mtaa, mdhamini na
kamishna wa viapo.; - Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla
ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao; - Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa
na Wakala w Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa
Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa
aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo; - Kwa mwombaji mwenye akaunti ya benki ajaze taarifa zake
kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo; - Kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho
cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa
kuomba mkopo. - Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa
mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.